Warsha ya makumbusho ya Alkafeel imerudisha uhai wa malikale mbili..

Maoni katika picha
Wataalamu wa makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekarabati malikale mbili za kubebea mishumaa (Sham’adani) niongoni mwa vifaa vya wakati wa utawala wa Othmaniyya, vilivyo tengenezwa mwaka 1300h.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa kama zawadi kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kupokelewa kazi ya kuvitengeneza ikaanza, kiongozi wa idara ya maabara Ustadh Hussein Ma’maar ametuhadithia kwa ufupi, amesema: “Hakika watumishi wa idara ya maabara wanaujuzi na uzowefu mkubwa wa kukarabati malikale, wamesha karabati malikale nyingi za madini na kawaida, zikiwemo malikale hizi”.

Akaongeza kuwa: “Ukarabati hupitia hatua nyingi, kama ifuatavyo:

  • - Kupiga picha pande zote za malikale.
  • - Kuandika vielelezo vya aina mbili, kwanza vielelezo vya kihandisi na pili vielelezo vya kihistoria ikiwa ni pamoja na umri wa kifaa na mwaka kiliotengenezwa na mengineyo.
  • - Hatua za matengenezo (kurepea) hupitia katika awamu mbili, kwanza kwa kutumia mikono na pili kwa kutumia kemikali, ili kurekebisha yasiyoweza kurekebishwa kwa mikono.
  • - Kusafisha kifaa kwa kutumia kemikali zinazo endana na aina ya kifaa.
  • - Kupaka rangi itakayo linda kifaa kisichakae na itakayo onyesha uhalisia wa kifaa husika”.

Akabainisha kuwa: “Baada ya kufanyika hayo hukamilika ukarabati wa vifaa, kama tulivyo fanya katika vifaa hivi vya kubebea mishumaa, na kuwa tayali kwa kuwekwa kwenye ukumbi wa maonyesho ya makumbusho”.

Akamaliza kwa kusema: “Ukarabati wa malikale unaofanywa na maabara yetu, hutimiza vigezo vyote vya makumbusho bila kuharibu hadhi yake kihistoria”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: