Mpiga picha wa kituo cha Alkafeel amepata tuzo nne kwenye mashindano mawili ya kimataifa

Maoni katika picha
Mpiga picha bwana Haidari Mankushi anaefanya kazi katika kituo cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu, amepata tuzo nne kwenye mashindano mawili ya kimataifa, amepewa midani ya dhahabu na kushinda makumi ya wapiga picha wa kimataifa walioshiriki kwenye mashindano hayo.

Zawadi ya kwanza aliyopokea ilikua ni kutoka shindano la kisiwa cha sheria za kimataifa PSA 2021M, lililofanywa Baharaini chini ya jumuiya ya kimarekani na taasisi zingine za kimataifa, kulikuwa na washindani (2500) kutoka nchi (48).

Kwenye shindano hilo amepata midani ya dhahabu katika upigaji wa picha za mnato za matukio ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), hali kadhalika akapata zawadi kutoka kwa kamati ya majaji na zawadi ya mashariki kwa kushiriki kwenye vipengele vingine vya shindano hilo.

Kamera ya Mankushi haikuishia hapo, bali iliendelea kushiriki katika shindano lingine la kimataifa, na kuwa mshindi wa kwanza kwenye shindano la Ashiqina, nalo ni shindano la kimataifa linalo andaliwa na “msanii wa Iraq” chini ya usimamizi wa taasisi ya Naharaini ya vijana na maendeleo endelevu, lilikuwa shindano maalum katika ziara ya Arubaini ya bwana wa mashahidi Abu Abdillah Hussein (a.s), lilikuwa na ushiriki mkubwa wa wapigapicha wa ndani na nje ya Iraq, ambao walipiga picha matukio ya ziara hiyo inayohudhuriwa na mamilioni ya watu.

Kumbuka ushiriki wa shindano hilo na kupata tuzo ni sehemu ya muendelezo wa tuzo ambazo amekua akipata mpigapicha huyo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa, kutokana na uzowefu alionao unamuwezesha kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda, pamoja na ushirikiano mkubwa anaopewa na viongozi wa kitengo, bila kusahau uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: