Kufungua mlango wa usajili katika mradi wa kitaifa wa Alkafeel wa Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya imefungua mlango wa usajili katika mradi wa masomo ya Qur’ani, unaohusisha semina mbalimbali za Qur’ani kwa wanaume tu, usajili utaendelea hadi siku ya Jumatano ya tarehe (12 Januari 2022m) kwa kujaza fomu kwa njia ya mtandao.

Semina za mradi:

 • - Hukumu za usomaji wa Qur’ani na tajwidi, chini ya ukufunzi wa Dokta Rafii Al-Aamiriy.
 • - Kusimama na kuanza, chini ya ukufunzi wa Dokta Muhammad Abdushakuru.
 • - Maarifa ya Qur’ani, chini ya ukufunzi wa Dokta Najahu Hasanawi.
 • - Njia za ufundishaji, chini ya ukufunzi wa Dokta Haidari Shallah.

Masharti ya kushiriki kwenye mradi:

 • 1- Muombaji asiwe na umri chini ya miaka mumi na nane, wala asizidi miaka arubaini na tano.
 • 2- Asiwe na elimu chini ya sekondari (upili).
 • 3- Awe na elimu ya awali ya hukumu za usomaji wa Qur’ani na tajwidi.
 • 4- Ahudhurie masomo yatakayofundishwa ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu kila siku ya Alkhamisi kuanzia saa nane baada ya Adhuhudi hadi saa kumi na moja kwa muda wa wiki thelathini.

Faida za mradi:

 • - Maahadi itatoa vyeti kwa wahitimu.
 • - Washindi wa tatu wa kwanza watapewa zawadi maalum na washiriki wote watapewa zawadi pia.
 • - Maahadi itatoa msaada maalum kwa wahitimu wa mradi wake na itawapa nafasi ya kushiriki kwenye miradi mingine mikubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: