Wito wa kushiriki kwenye nadwa ya pamoja kati ya Ataba mbili tukufu ya Radhwawiyya na Abbasiyya

Maoni katika picha
Kituo cha upigaji picha nakalakale na faharasi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa wito wa kushiriki katika nadwa ya kielimu itakayofanywa kwa kushirikiana na kituo cha Atabatu Ridhwawiyya takatifu.

Nadwa itafanywa kwa njia ya mtandao chini ya anuani isemayo: (Atabatu Abbasiyya ya Atabatu Radhwawiyya ni njia mpya ya watafiti.. kitengo cha uthibitishaji na picha cha Atabatu Abbasiyya na Atabatu Radhwawiyya ni mfano katika hilo).

Kutakuwa na makabidhiano ya mada za kitafiti, atabatu Abbasiyya itawakilishwa na mkuu wa kituo Ustadh Swalahu Siraji, atatoa ufafanuzi kuhusu vifaa vya kituo na namna wanavyo tunza nakala-kale katika Ataba tukufu, pamoja na kiongozi wa kitengo cha uthibitishaji katika kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi, Ustadh Muhammad Baaqir Zubaidi chini ya anuani isemayo: (uthibitisho wa kihistoria katika stoo ya Atabatu Abbasiyya tukufu).

Kutoka Atabatu Radhwawiyya takatifu atakua Ustadh Muhammad Haadi Zaahidi mkuu wa uthibitishaji na machapisho, na Ustadhat Aaliha Mahbuub kiongozi wa kitengo cha uthibitishaji.

Kumbuka kuwa nadwa hiyo ni muendelezo wa nadwa zinazofanywa na maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na vituo vilivyo chini yake, kulingana na uhusika wa kila kituo, hupata muitikio mkubwa kutoka kwa wasomi na wadau.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: