Mahudhurio ya kwanza ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Ambaar kupitia shirika la Khairul-Juud kwenye tamasha la kibiashara

Maoni katika picha
Shirika la Khairul-Juud la teknolojia ya viwanda na kilimo cha kisasa, limekua daraja la ushiriki wa kwanza wa Atabatu Abbasiyya kwenye shughuli za mkoa wa Ambaar, kwa kushiriki kwenye tamasha la kibiashara la kitaifa na kimataifa.

Wameshiriki wakiwa na zaidi ya bidhaa (100) za aina mbalimbali kama vile mbolea, nafaka, dawa pamoja na barakoa na vitakasa mikono, zilizotengenezwa na mikono ya wairaq zinazo lenga kuboresha uzalishaji wa ndani na sekta ya kilimo.

Mhandisi Falahu Fatla mkuu wa masoko ya mbolea na bidhaa za kilimo katika shirika ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika shirika la Khairul-Juud linawajali sana raia wa Iraq, kupitia vituo vyake vya mauzo vilivyopo mikoani, au kupitia maonyesho na makongamano ambayo nisehemu muhimu ya kujitangaza, likiwemo tamasha hili la kibiashara katika mkoa wa Ambaar ambalo tunashiriki kwa mara ya kwanza”.

Akaongeza kuwa: “Tumepewa mapokezi maalum na kamati ya maandalizi ya kongamano, tawi la shirika limekuja na bidhaa mbalimbali za kilimo kama vile mbolea na dawa za mimea ambazo ni rafiki kwa mazingira na zinazo kidhi viwango vya kimataifa, mbolea tunazo za aina tofauti, kavu na za maji zinazofaa kwa aina tofauti za mazao, aidha tumekuja na aina tofauti za vyakula vya wanyama”.

Akaendea kusema: “Tumekuja pia na aina mbalimbali za vitakasa mikono na barakoa zinazofaa kwa matumizi ya nyumbani, kiwandani na hospitali”.

Akasisitiza kuwa: “Tangu kufunguliwa kwa tamasha hili, tumeshuhudia muitikio mkubwa wa watu wa Ambaar, kwani walikua wamesha sikia kuhusu bidhaa zetu lakini walikua hawajapata nafasi ya kuziona, hivyo tamasha hili imekua fursa kwao ya kuziona”.

Akamaliza kwa kusema: “Ushiriki wetu pia umetupa nafasi ya kujuana na mashirika mengine ya biashara, na mengine yameomba uwakala katika mikoa yao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: