Kuangazia kumbukumbu ya kifo cha mwenye karama Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s)

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na mbili Jamadal-Awwal ni siku ya kumbukumbu ya huzuni kubwa kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wapenzi wao na wafuasi wao katika mwaka wa 192h, alifariki dunia mwenye karama Qassim mtoto wa Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s), kutokana na kumbukumbu hiyo tutaeleza machache kuhusu Maisha yake matukufu.

Riwaya zinaonyesha kuwa Qassim (a.s) alihama katika mji wa babu yake Mtume (s.a.w.w) na kwenda Iraq pamoja na msafara wa wafanya biashara, kama sehemu ya kujilinda na shari za watawala waliokuwa wakimnyanyasa Imamu Alkaadhim (a.s), kutokana na kuendeleza kwake familia ya Mtume na kuwa kisima cha hekima na chemchem ya elimu na upole kwa waumini, watawala waliwanyanyasa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), jambo lililopelekea watoto wa Imamu Mussa (a.s) kusambaa kila sehemu ya dunia, akiwemo Imamu Ridhwa (a.s) na Qassim (a.s) ajulikanae kwa elimu na ukomavu wa akili yake.

Qassim (a.s) alifariki baada ya ugonjwa mkubwa aliougua mwaka (192h) katika mji wa Sura mtaa wa Bakhamra, sehemu lilipo kaburi lake tukufu lililojengewa kubba la dhahabu na minara mikubwa hivi sasa.

Miongoni mwa wasia wake (a.s) kwa Ammi yake Shekh Hayu aliyeoa mmoja wa mabinti zake, alisema: (Ewe Ammi.. nikifa nioshe univishe sanda na kunizika, ukifika wakati wa hija nenda kahiji pamoja na binti yako na huyu binti yangu, mtakapo maliza ibada ya hija nendeni Madina, mkifika kwenye lango la Madina mshushe binti yangu atembee na nyie mtembee nyuma yake, hadi atakapo fika katika nyumba ndefu akasimama, hiyo ndio nyumba yetu, mtaingia hapo na kuwakuta wanawake wote wajane).

Mwaka wa pili baada ya kifo cha Qassim (a.s) Shekh Hayu alikwenda hija pamoja na binti wa Qassim (a.s), ikawa kama alivyo sema Qassim (a.s), binti yake alienda hadi katika nyumba na kugonga mlango, akafunguliwa na kuzungukwa na wanawake wa Hashimiyya, wakamuuliza jina lake na hali ya baba yake, akalia, mama yake Qassim (a.s) alipotoka ndani na kumuangalia mtoto yule alianza kuita: ewe mwanangu, ewe Qassim wangu.. wallahi huyu ni yatima wa Qassim, kisha yule binti akawaambia kuwa mama yake na babu yake wamesimama nje ya nyumba, inasemekana mama yake Qassim baada ya kusikia kifo cha mwanae aliugua na akafa baada ya siku tatu.

Qassim (a.s) alikua miongoni mwa watu watukufu katika familia ya Mtume (s.a.w.w) na alikua mfasaha zaidi baada ya kaka yake Imamu Ridhwa (a.s), yatosha kueleza utukufu wake kupitia riwaya iliyopokewa na Shekhe Kuleini katika kitabu cha Usulul-Kaafi mlango wa Nassu: kutoka kwa Imamu Ali bun Mussa Ridhwa (a.s) kutoka kwa Yazidi bun Saliit kutoka kwa Imamu Kaadhim (a.s) walipokua katika njia ya Maka Imamu alisema: (…Nilikuambia ewe Abu Ammarah, nilitoka katika nyumba yangu nikamuhusia mwanangu fulani na nikamshirikisha mwanangu fulani, nikamuambia akiwa peke yake, kama ingekua jambo (la Uimamu) liko mikononi mwangu ningempa mwanangu Qassim kutokana na mapenzi yangu kwake, lakini maamuzi ni ya Mwenyezi Mungu mtukufu anampa amtakae).

Malalo ya Qassim (a.s) yapo umbali wa farsakh nane kutoka Hilla (makao makuu ya mkoa wa Baabil), hutembelewa na watu wote, ziara yake inaumaalum wake, Sayyid ibun Twausi amehimiza kumzuru kwenye kitabu chake cha Misbaahu-Zaairu, ameeleza ziara ya Qassim mtoto wa Imamu Alkaadhim (a.s) pamoja na ziara ya Abulfadhil Abbasi mtoto wa Imamu Ali kiongozi wa waumini (a.s) na Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s), katika mlango usemao: (Kutaja ziara za watakatifu watoto wa Maimamu (a.s), ukitaka kumzuru mmoja miongoni mwao kama vile Qassim bun Alkaadhim, Abbasi bun Amirulmu-uminina, Ali bun Hussein (a.s) aliyeuawa Twafu, kuna hadithi kutoka kwa Imamu Ridhwa (a.s) anasema: (Atakaeshindwa kunizuru basi amzuru ndugu yangu Qassim).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: