Kuratibu warsha ya kielimu kuhusu fani ya malezi na athari yake katika kubadilisha tabia za wanafunzi

Maoni katika picha
Jumuiya ya kielimu Al-Ameed kwa kushirikiana na shule za Al-Ameed, imefanya warsha ya kielimu kuhusu malezi iliyopewa jina la (Fani ya malezi na athari yake katika kubadilisha tabia za wanafunzi), warsha hiyo ni maalum kwa watumishi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa lengo la kukuza uwezo wao na kuwaongezea maarifa ya malezi na kuamiliana na wanafunzi.

Warsha hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa mikutano katika jengo la makao makuu ya jumuiya, mtoa mada alikua ni kiongozi wa idara ya maelekezo katika kitengo cha malezi na elimu ya juu Ustadh Falahu Hassan Juma.

Katika warsha hiyo yamezungumzwa mambo muhimu, miongoni mwa mambo hayo ni: Fani ya malezi katika kushirikiana na walimu na kubaini tabia nzuri na mbaya, walianza kutambulisha tabia kisha kuainisha aina zake na baada ya hapo vikatambulishwa vipimo vya tabia, pamoja na mielekeo mikuu inayotumiwa na wataalamu wa malezi katika kubadili tabia za wanafunzi.

Mtoa mada ya warsha ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa washiriki, wameonyesha shauku ya kujifunza mbinu za kubadilisha tabia za wanafunzi, kwani wanafanya kazi hiyo kwa sababu wao ni walimu, wanakutana na wanafunzi wenye tabia nzuri na mbaya, hivyo wanajukumu la kubadilisha tabia mbaya za wanafunzi wao na kuwafanya wawe na tabia nzuri”.

Kumbuka kuwa jumuiya ya kielimu Al-Ameed imesajiliwa rasmi katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, tarehe 24/7/2019m, chini ya kifungu cha wizara namba BT 2 – 7199, harakati zake zote zinasimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: