Ataba mbili Radhwawiyya na Abbasiyya zimeratibu semina ya kutambua vituo malikale za kihistoria

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Radhwawiyya na Abbasiyya zimefanya semina kwa njia ya mtandao, ya kutambua vituo vya kihistoria na kuangazia malikale za Ataba mbalimbali, mbele ya watafiti na wadau wengi, semina hiyo ilikua na anuani isemayo: (Malikale za Atabatu Abbasiyya na Atabatu Radhwawiyya ni njia mpya ya watafiti.. kitengo cha malikale cha Atabatu Abbasiyya na kituo cha malikale cha Atabatu Radhwawiyya kama mfano).

Nadwa imefunguliwa kwa ujumbe wa mkuu wa upigaji picha nakala kale na faharasi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Swalahu Siraji, ametaja hatua zilizochukuliwa na Ataba tukufu katika kuhifadhi turathi na nakala kale, na mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo, pamoja na vifaa vya kisasa wanavyo tumia ambavyo ni msaada mkubwa katika kutunza turathi za kiislamu.

Ukafuata ujumbe mwingine kutoka kwa mkuu wa kituo cha nakala kale na machapisho katika Atabatu Radhwawiyya Ustadh Muhammad Haadi Zaahidi, alianza kwa kukaribisha washiriki na kuishukuru Atabatu Abbasiyya kwa ushiriki wake, akasifu pia kwa kazi kubwa inayofanya ya kutunza turathi na nakala-kale.

Hali kadhalika kulikua na mada ya kitafiti katika nadwa hiyo, iliyowasilishwa na mkuu wa kitengo cha malikale na kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi Ustadh Muhammad Baagir Zubaidi, mada yake ilikua inasema: (Malikale za kihistoria katika stoo za Ataba, maonyesho na uchambuzi), ametaja mtazamo wa kihistoria na jinsi ya kuufanyia kazi.. na akaonyesha baadhi ya vifaa vya kihistoria na kufafanua njia inayotumiwa na Atabatu Abbasiyya kupitia program ya kielekronik, hali kadhalika akaonyesha mifano ya vifaa vya kihistoria vilivyopo katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akabainisha umuhimu wake na kazi iliyofanywa ya kuzihifadhi na kuzifanya kuwa msingi wa tafiti za kielimu.

Nadwa hiyo imeshuhudia maoni na michango kutoka kwa washiriki, watoa mada wamefafanua zaidi pale palipo hitajika, bila kusahau kulikuwa na mada kutoka kwa Ustadhi Muhammad Haadi Zaahidi mkuu wa malikale na machapisho katika Atabatu Radhwawiyya, na Ustadhat Aaliha Mahbuub kiongozi wa kitengo cha malikale katika Atabatu Radhwawiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: