Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza zaidi ya mita elfu moja katika mazaru ya Sayyid Ismaeel Karbala kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameongeza eneo lenye ukubwa wa mita (1250) kwenye malalo ya Sayyid Ismaeel mashariki ya Karbala, umbali wa kilometa sita, kwa lengo la kuongeza eneo la kupumzika mazuwaru wake na kuongeza uzuri wa sehemu hiyo.

Kiongozi wa idara ya mitambo na ujenzi katika kitengo tajwa na msimamizi mkuu wa kazi hiyo Ustadh Hassan Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na maombi ya mazaru, kitengo chetu kimeunda kikosi kazi kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya kupumzika mazuwaru, kutokana na udogo wa eneo hilo ambalo hupokea idadi kubwa ya mazuwaru, huku eneo la kupumzika na kufanya ibada likiwa dogo”.

Akaongeza kuwa: “Hatua ya kwanza tumefanya uchambuzi na kuainisha sehemu inayokusudiwa kuongezwa na kubaini matumizi yake, kisha tukaanza kuisawazisha na kuondoa udongo usiofaa na kuweka aina ya udongo unaofaa kuotesha mimea kwa ajili ya kutengeneza bustani inayokadiriwa kuwa na ukubwa wa mita (960) na kuweka lami sehemu za njia”.

Abdulhussein akabainisha kuwa: “Eneo lililo ongezwa limehusisha njia zenye upana wa mita nne, na eneo la wazi mita (200) na sehemu ya bustani, na sehemu ya kupumzika, umewekwa mfumo wa umwagiliaji pia”.

Kumbuka kuwa kazi hii ni sehemu ya shughuli za Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhudumia watu wa Karbala na mazuwaru, ambapo hufanya ujenzi au ukarapati wa majengo ya umma, taasisi na mazaru tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: