Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil imemaliza kuandaa mpango mkakati wake wa mwaka

Maoni katika picha
Kamati ya elimu katika Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeandaa mpango mkakati maalum wa tawi.

Kiongozi wa tawi la Maahadi Sayyid Muntadhiru Mashaikhi amesema: “Miradi iliyopangwa itatekelezwa ndani ya muta uliowekwa, kulingana na aina ya mradi”, akaongeza kuwa: “Mpango mkakati unaprogram nyingi za Qur’ani sambamba na kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu”. Akasisitiza kuwa: “Mpango mkakati hauishii katika tawi la Baabil peke yake, bali umehusisha wilaya na vitongoji vingine”.

Tambua kuwa tawi la Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Baabil, hufanya harakati tofauti za Qur’ani tukufu, sambamba na semina za Qur’ani endelevu hapa mkoani.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu kwenye Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inawajibu wa kufundisha Qur’ani na kuandaa jamii yenye uwelewa wa fani tofauti za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: