Kufanyika kongamano la turathi la kumi na tatu na kuweka mazingira ya (Itikadi za Imamiyya) kwenye meza ya majadiliano

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya kwenye ukumbi wake mkuu, limefanyika kongamano la kumi na tatu la kujadili (Idikadi za Imamiyya: kwa mujibu wa kitabu cha Allamah Hilliy mlango wa kumi na moja), mtoa mada alikua Mheshimiwa Sayyid Izu-Dini Alhakiim mbele ya wasomi wa Dini na sekula na wanajamii.

Kongamano limefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha ukafuata ujumbe wa kituo uliowasilishwa na Shekh Swadiq Khawilidi, uliyokua inasema mchango wa turathi za Hilla na wanachuoni wake katika uandishi wa vitabu vya kishia, akiwemo Sayyid Hakiim.

Baada ya hapo Sayyid Hakiim akawasilisha huduba yake ambayo alianza kwa kueleza mchano wa Hilla katika elimu, kisha akataja fikra muhimu zilizopo katika itikadi ya madhehebu ya Imamiyya, akaeleza changamoto zilizopo kwa karne nyingi katika madhehemu hiyo, na namna wanachuoni wa madhehebu walivyo pambana na kujitolea kila kitu kwa ajili ya kufundisha misingi sahihi, akatumia kitabu za Allamah Hilliy (mlango wa kumi na moja) kama mfano wa maelezo yake.

Kongamano limepambwa na maoni na maswali kutoka kwa wasomi wa hauza na sekula, kuhusu itikadi ya sasa na zamani.

Kongamano limeshuhudia usomwaji wa kaswida ya kishairi, iliyosomwa na mshairi Swalahu Lubani kutoka Hilla lililobeba ujumbe wenye maana na fikra nzuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: