Kufanikiwa upandikizaji wa mboni ya jicho kwa mtoto mwenye umri wa miaka 10

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel mjini Karbala, limetangaza kufanikiwa kwa upandikizaji wa mboni ya jicho kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10.

Daktari bingwa wa macho katika hospitali hiyo Dokta Salaam Qar’awi amesema: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kupandikiza mboni ya jicho ya aina ya (trifocal IOL), kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka (10) pamoja na kuondoa weusi”, akafafanua kuwa: “Kazi hiyo imefanywa kwa weledi mkubwa ndani ya jicho la mgonjwa”.

Akasisitiza kuwa: “Mtoto ameweza kuona vizuri mbali na karibu bila kutumia miwani, upasuaji huo umetumia dakika (10) tu”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel imekuwa ikifanya juhudu ya kutoa huduma bora kwa kutumia vifaa vya kisasa wakati wote, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi na wauguzi mahiri, jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila wakati sambamba na kupokea wagonjwa mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: