Makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya imeanza kufanya nadwa kuhusu makumbusho zinazo lenga kutambulisha turathi za kitamaduni, na namna ya kuzihifadhi kwani ni sehemu ya utambulisho wetu.
Nadwa ya kwanza ilikua na anuani isemayo: (Kumbukumbu za turathi baina ya uelewa na utambuzi), imefanywa kwa wajumbe kuhudhuria ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu, na kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (ZOOM), ambapo idadi kubwa ya wadau wa makumbusho wameshiriki nadwa kwa kutumia njia hiyo.
Mtoa mada wa nadwa hii ni rais wa kitengo cha makumbusho Dokta Shauki Mussawi, ameongea kuhusu kumbukumbu za turathi baina ya uwelewa na utambuzi, akasisitiza kuwa maswala ya turathi ni muhimu sana kwetu na tunatakiwa kuyatunza, hali kadhalika ameongea kuhusu vifaa vya kutunzia turathi na misamiati ya kilugha inayotumika katika turathi.
Akasema hisia ya jicho inaongea kuhusu hisia ya vita katika turathi, kuanzia jamii za zamani hadi zama za kati na zama za sasa tulizopo, mfano wa hilo ni yale yaliyofanywa na magaidi wa Daesh, kuchoma, kuvunja na kujaribu kufuta kabisa utambulisho wa turathi.
Akaongea pia kuhusu ulazima wa kujali turathi, kwani ni utunzaji wa kumbukumbu za babu zetu ambao ndio utambulisho wetu, tunatakiwa kujua kuwa turathi ndio heshima ya utamaduni, maarifa, uzuri, tabia katika maisha ya vizazi na umma zilizo tangulia.
Naye rais wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Nadwa hii ni sehemu ya maazimio ya kongamano la makumbusho ya Alkafeel la kimataifa la awamu ya tatu, lililo himiza kujali sekta ya utamaduni na makumbusho, kwa lengo la kulinda turathi zetu na utambulisho wetu wa kiarabu na lugha yetu pamoja na kubaini changamoto zinazo kumba turathi zetu, nadwa hizi zitasaidia kuzungumza mambo tuliyokua hatujaongea siku za nyuma kwa ajili ya kuhifadhi turathi zilizopo kwenye makumbusho ya Alkafeel au taasisi za kijamii”.
Akafafanua kuwa: “Makumbusho ni sawa na kitabu kilicho andikwa mafanikio ya vizazi vilivyo pita kwenye sekta tofauti, yanamchango mkubwa katika kuonyesha utambulisho wa watu na maendeleo yao kwa vizazi vingine, aidha ni njia ya mawasiliano ya umma na kujenga uzalendo wa taifa, nadwa hizi zinasaidia kuangazia mambo hayo”.
Kumbuka kuwa tumeweka ratiba ya nadwa hizi ambapo tutajadili mambo mbalimbali yanayo husu utamaduni na makumbusho, kila mwezi tutafanya nadwa moja au zaidi.