Kuanza shindano la (Hazina ya maarifa) la kila mwezi na kutoa zawadi kwa washindi

Maoni katika picha
Kituo cha elektronik na taaluma chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuanza kwa shindano la kila mwezi la kielekronik lenye anuani isemayo: (Hazina za maarifa) pamoja na kutoa zawadi kwa washindi.

Shindano hili ni sehemu ya harakati za kituo cha kitamaduni kwa ujumla, na kuongeza maarifa kwa washiriki, katika mambo mbalimbali ya kibinaadamu, linahusisha kuuliza maswali yatakayo jibiwa kupitia link ifuatayo: http://almerja.com/knoze/

Kituo kimeandaa zawadi tatu kwa washindi watatu wa mwanzo, iwapo wakifungana basi itapigwa kura ili kupata washindi watatu, zawadi zao zitakua kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: (100,000 dinari za Iraq) + pete ya fedha.

Mshindi wa pili: (75,000 dinari za Iraq) + pete ya fedha.

Mshindi wa tatu: (50,000 dinari za Iraq) + pete ya fedha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: