Kundi la wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya wanahitimisha mwaka wao wakiwa ndani ya haram za Ataba mbili tukufu

Maoni katika picha
Kundi la wanafunzi wa chuo kikuu cha Mustanswiriyya wamehitimisha mwaka wao wakiwa ndani ya haram za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa kufanya ziara siku ya Ijumaa (26 Jamadal-Uula 1443h) sawa na tarehe (31 Desemba 2021m).

Wamepokewa na idara ya uhusiano wa vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuwaandalia ratiba maalum iliyokua na vipengele vingi, mtandao wa Alkafeel umeongea na Ustadh Mustwafa Alkaadhimi, amesema: “Kupokea ugeni wa wanafunzi ni sehemu ya ratiba yetu ya kupokea wanafunzi wa vyuo, ratiba hiyo mwaka huu imehitimishwa kwa kupokea wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya, waliotamani kumaliza mwaka wakiwa ndani ya haram ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kupokea wageni, tumewaeleza malengo ya ratiba hii na mafanikio yake pamoja na kufafanua ratiba ya mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel ambao unaendeshwa na idara yetu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba ilifunguliwa kwa kutembelea vitalu vya Atabatu Husseiniyya tukufu na majengo ya makazi ya Abbasi (a.s), pamoja na kuwasilishwa mihadhara miwili, mmoja ulikua na anuani isemayo: (Namna ya kutunza utambulisho wa taifa), na mwingine unasema: (Kujibu changamoto za sasa na namna ya kujilinda nazo), kisha wakatembelea kitengo cha zawadi na nadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, makumbusho ya Alkafeel, kituo cha biashara Al-Afaaf”.

Akasema: “Matembezi hayo yalihitimishwa kwa kufanya ziara ya pamoja katika malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha tukawaaga wageni kama tulivyo wa karibisha na kuwaombea dua za mafanikio”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: