Mazuwaru wanaanza siku ya kwanza katika mwaka mpya wa Miladi wakiwa ndani ya Ataba mbili tukufu

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu usiku wa jana na leo, zimeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru pamoja na ugumu wa hali ya hewa, wanakuja kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuifanya siku yao ya kwanza katika mwaka mpya wa miladi (2022) kuitumia wakiwa katika eneo hili takatifu lenye mazingira mazuri ya kiroho na mafundisho ya Ahlulbait (a.s).

Ziara hii inasaidia kuhuisha moyo kiimani na kuwa tofauti na sherehe zingine, wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu na kutafuta shifaa ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu alilinde taifa la Iraq na kila aina ya shari katika mwaka huu, atuepusha na ubaya wa usiku na mchana na atuweke chini ya ulinzi wake, atuondolee maadui na atupandishe daraja na atubariki katika kila kitu.

Katika mazingira hayo mazuri kiimani na kwa ajili ya kurahisisha ufanyaji wa ziara hiyo, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeweka mazingira mazuri na kuimarisha usalama kwa ajili ya kuhakikisha mazuwaru watukufu wanafanya ibada zao kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: