Maahadi ya Qur’ani tukufu inafanya mkutano mkubwa wa kujadili mkakati wake mpya

Maoni katika picha
Kamati ya Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani inafanya mkutano wa kujadili mkakati wa mwaka kesho kwa ajili ya kujipanga kuutekeleza kama ulivyo pangwa na kwa wakati ulio wekwa, kwa mujibu wa malengo yanayokusudiwa.

Mkutano huo umehusisha rais wa kamati Shekhe Jawadi Nasrawi na wajumbe wa kamati ya Maahadi, wakiwemo viongozi wa matawi na idara za kielimu, pamoja na viongozi wa idara mbalimbali.

Katika kikao hicho wajumbe wametaja mambo waliyofanya mwaka huu, na kupitisha mkakati mpya na kugawana majukumu, sambamba na kuwajulisha watumishi wote mambo ambayo Maahadi inakusudia kuyafanya katika sekta ya Qur’ani, ili waweze kuchangia utekelezaji wa mkakati huo kwa ukamilifu.

Katika mkutano huo, umeandaliwa mpango kati utakao tangazwa hivi karibuni, utatumika Karbala na mikoani, unahusisha watu wenye umri tofauti, unalenga kuboresha kiwango cha elimu na usomaji wa Qur’ani katika taifa letu kipenzi la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: