Baina ya haram mbili tukufu pashuhudiwa maonyesho ya mabango yaliyochorwa yaliyojiri kwa Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu umeshuhudia maonyesho na maigizo yanayo angazia maisha ya bibi Zaharaa (a.s), kufuatia kumbukumbu ya kifo chake (a.s).

Maigizo yamefanywa kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya na kitengo kinasho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, chini ya kamati ya maigizo ya Tufuuf-Husseiniyya kutoka mkoa wa Basra, na kuhudhuriwa na watu wengi miongoni mwa mazuwaru.

Washiriki wa maonyesho wametengeneza maigizo kwa kutumia vitabu vya historia vinavyo kubalika katika kueleza historia ya bibi Zaharaa (a.s), na mambo yaliyotokea baada ya kifo cha baba yake Mtume mtukufu (s.a.w.w).

Wasimamizi wa maonyesho hayo wamezingatia manufaa ya maigizo katika kumtambulisha mama hiyu mtakatifu, sambamba na kuonyesha baadhi ya dhulma alizo fanyiwa.

Igizo limepambwa na sauti za wahadhiri wa mimbari ya Husseiniyya, wanao zungumza majonzi ya Ahlulbait (a.s) na kifo za bibi Zaharaa (a.s).

Kumbuka kuwa katika siku kama hizi kila mwaka huwa tunazungumza kuhusu kifo cha mtukufu wetu Swidiqah Shahidah Fatuma Zaharaa (a.s), hakika amekua na vipindi tofauti vya kukumbuka kifo chake (a.s) kutokana na kutofautiana kwa riwaya zinazotaja tarehe ya kifo chake, riwaya mashuhuri zaidi zipo tatu, ndizo ambazo hutumiwa kuomboleza kifo cha bibi Fatuma (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: