Atabatu Abbasiyya inaangalia uzowefu wa mradi wa vyumba tambuzi kwa ajili ya huduma za matibabu

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inaangalia uzowefu wa mradi wa vyumba tambuzi katika kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, kupitia warsha za kielimu zinazofanywa katika chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Ataba tukufu, wajumbe wamehudhuria kwenye warsha ndani ya ukumbi wa mikutano na wengine wameshiriki kwa njia ya mtandao kupitia jukwaa la (zoom).

Warsha imeratibiwa na jumuiya ya kielimu Al-Ameed kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa Alkafeel, chini ya uhadhiri wa Abdullahi Hamudi Albadri anayefanya kazi katika kamati ya afya ya Dubai/ mada yake ilikua inasema: (Ufafanuzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba tambuzi).

Mtoa mada amefafanua umuhimu wa kujenga vyumba tambuzi na namna ya kuweka mazingira salama kwa mgonjwa, hospitali nyingi katika nchi zilizo endelea wanatumia mfumo huo -vyumba tambuzi- wanatoa huduma kwa kutumia teknolojia sambamba na uboreshaji wa huduma za afya.

Baada ya hapo akaashiria kuwa teknolojia hii ni ya kisasa na muhimu, inasaidia kuimarisha ulinzi wa afya ya ngonjwa, kwa kutumia njia za utambuzi katika kutoa tiba, inafaida nyingi, kama vile ufanyaji kazi wa kifaa tiba kwa njia ya mtandao, na kuandika maelezo kwa kutumia mfumo.. na mengineyo.

Mwisho wa warsha kulikua na maoni mengi na maswali kuhusu vyumba tambuzi, mtoa mada amejibu maswali yote na kufafanua zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: