Fani ya kuandika kisa kifupi katika jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia idara ya jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s), imefanya semina ya (fani ya uandishi wa kisa kifupi) kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Zaharaa (a.s).

Semina hii ni matokeo ya ushirikiano wa vyuo na kuboresha mawakibu na uwezo wa wanafunzi katika sekta hii adhim ya uandishi, watumishi wa jarida wanauzowefu mkubwa katika jambo hilo.

Nayo ni moja ya semina ambazo zimekua zikitolewa kwa wiki mbili sasa, chini ya ukufunzi wa muandishi wa jarida hilo bibi Dalali Kamali Akiliy, amezungumza mada nyingi, kama vile madhumuni ya kisa kifupi na uandishi wake, maelezo kuhusu aina za adabu kihistoria, namna ya uandishi unaotimiza vigezo.

Amesherehesha pia namna ya kuweka madhumuni na mtazamo kwenye kisa kifupi, akaonyesha visa mbalimbali vilivyo andikwa kwenye jarida la Riyaadhu-Zaharaa (a.s) na majarida mengine, na kujadili nguzo zake na lugha yake na kila changamoto inayoweza kutokea katika uandishi.

Nadwa imepata muitikio mkubwa kutoka kwa washiriki walioanza kuandika visa vifupi, kama sehemu ya kufanyia kazi mambo waliyofundishwa kwa nadhariyya kwenye semina hiyo.

Mwishoni mwa semina, mkuu wa kitivo cha malezi ametoa shukrani kwa maktaba na wakufunzi wa semina akaomba ushirikiano uendelee na kwenye sekta zingine pia.

Kumbuka kuwa semina hii ni sehemu ya ushirikiano wa kitamaduni pamoja na chuo kikuu cha Zaharaa (a.s) kwa lengo la kutoa elimu kupitia maktaba ya Ummul-Banina (a.s) ya wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: