Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu imepekea wageni kutoka taasisi ya Saidi bun Jubairi ya Qur’ani katika mkoa wa Waasit.
Ziara hii ni sehemu ya kukuza ushirikiano baina ya pande mbili, baada ya kukaribishwa wageni kimefanywa kikao cha usomaji wa Qur’ani tukufu.
Kikao hicho kimefunguliwa kwa Qur’ani iliyosomwa na msomaji wa tawi bwana Maitham Farjawi, ukafuata ukaribisho uliotolewa na muwakilishi wa tawi Ustadh Dhiyaau Waziri, akaeleza miradi na harakati zinazofanywa na Maahadi, ikiwa ni pamoja na semina, nadwa, kuhifadhisha Qur’ani na vikao vya usomaji wa Qur’ani.
Rais wa taasisi hiyo Dokta Twariq Zarkani ameshukuru idara ya Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’ani, kwa kazi kubwa wanayo fanya katika sekta ya Qur’ani, na kutoa mafundisho ya vizito viwili kwa wanajamii.
Kikao hicho kimeshuhudia maonyesho ya baadhi ya vipaji vya kuhifadhi Qur’ani, vilivyo onyeshwa na baadhi ya wanafunzi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, ikiwa ni pamoja na kutaja aya za mwanzo wa sura, namba za aya na aya za mwisho wa sura, mbele ya walimu na wanafunzi wa tawi la Maahadi na taasisi.