Mradi wa ufugaji wa kware umeingiza sokoni kware laki mbili na elfu hamsini (250,000) na zaidi ya mayai milioni moja ndani ya mwaka mmoja

Maoni katika picha
Idara ya mradi wa ufugaji wa kware ni moja ya miradi ya shirika la uchuni Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, katika mwaka uliopita (2021) umefanikiwa kuingiza sokoni kware laki mbili na elfu hamsini (250,000) na mayai zaidi ya milioni moja, kupitia vituo vya biashara vilivyopo katika mkoa wa Karbala.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha kilimo katika shirika tajwa Mhandisi Ali Maz’ali Laaidh, akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya tukufu inamiradi mingi ya viwanda, kilimo na ufugaji inayo changia uzalishaji wa taifa, na kupunguza mahitaji ya kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi, miongoni mwa miradi yenye manufaa ni mradi wa kware, ambao ni miongoni mwa miradi ya kimkakati na mradi wa kwanza hapa Iraq”.

Akaendelea kusema: “Tangu ulipoanzishwa mradi huu tumeweka mkakati wa uboreshaji, kwa ajili ya kuongeza kiwango cha uzalishaji wa nyama za kware na mayai, kwani mahitaji ni makubwa kwa raia wa Iraq, tumepata matokea mazuri kutokana na mbinu za kisasa tunazo tumia, kuanzia kwa kware wanao totoa, utotoleshaji wa mayai hadi kuwafikia walaji”.

Akafafanua kuwa: “Mwaka jana kilikua kipindi cha kujipima kufikia malengo yaliyowekwa, na tulifanikiwa katika sekta ya uzalishaji, tunatarajia mwaka huu tutafikia matarajio yetu pia, tutaongeza kumbi nne za ufugaji wa kware, na kuboresha kumbi za kutotoleshea na mashine za kutotolesha, hadi tufikie uwezo wa kila ukumbi kutotolesha mayai (13000) hadi (17000)”.

Akahitimisha kwa kusema: “Kuna muitikio mkubwa wa watumiaji wa bidhaa zetu, nyama na mayai, kuna mahitaji makubwa sana, kwani bidhaa hizi ni nzuri kwa afya, na tunajitahidi zipatikane kwenye vituo vyote vya uuzaji vilivyo chini ya shirika la kibiashara Alkafeel”.

Kumbuka kuwa mradi unafanywa kwenye eneo lenye ukubwa wa mita za mraba (10,000), katika barabara ya (Najafu – Karbala), kuna kumbi nyingi za ufugaji wa kware na utunzaji wa mayai, hali kadhalika kuna sehemu maalum za kutunzia kware na mayai pamoja na kiwanda cha kutengeneza chakula cha kware kinacho zalisha tani moja kila siku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: