Maahadi ya Qur’ani tawi la Bagdad inafanya semina ya hukumu za Qur’ani na tajwidi kwa wanafunzi wanao anza

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la mji mkuu wa Bagdad, inafanya semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani na tajwidi kwa wanafunzi wanao anza.

Ustadh Ali Abbasi Khalidi mmoja wa walimu wa tawi amesema: “Maahadi imeratibu semina ya hukumu za usomaji wa Qur’ani na tajwidi kwa wanafunzi wanao anza kwenye kitongoji cha Jamila pembeni ya Raswafa kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (45).

Khalidi akabainisha kuwa: “Semina hufanywa kila siku ya Ijumaa katika msikiti wa bwana Majisar-Baidwani, chini ya usimamizi wa mwalimu wa Maahadi, na hufundishwa mada tofauti za Qur’ani, sambamba na semina zinazo fanywa katika kitongoji cha Karkhi na Raswafa, kwa lengo la kujenga uwelewa wa Qur’ani katika jamii”.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na harakati mbalimbali za Qur’ani, kwa lengo la kujenga uwelewa wa kitabu cha Mwenyezi Mungu katika jamii.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani ni kituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, yenye jukumu la kufundisha elimu ya Qur’ani na kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika mambo mbalimbali yanayo husu Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: