Wanafunzi wa chuo kikuu cha Alkafeel wameandaa soko la hiyari kwa ajili ya kusaidia taasisi ya Ain

Maoni katika picha
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameandaa soko la hiyari katika uwanja wake wa katikati, kwa ajili ya kusaidia taasisi ya Ain ya kulea mayatima, soko holo litadumu kwa muda wa siku mbili.

Soko hilo limefunguliwa na rais wa chuo cha Alkafeel Dokta Nurus Dahani, chini ya usimamizi wa kitengo cha maelekezo ya nafsi na muongozo wa malezi, nalo ni sehemu ya harakati za kitamaduni za kusaidia makundi ya wananchi wa Iraq, soko limesheheni mavazi, michoro, kazi za mikono, vitabu na vyakula.

Rais wa kitengo tajwa Dokta Husam Ali Hassan Ubaidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo chetu kina harakati nyingi, ikiwa ni pamoja na hili soko la hiyari ambalo ni sehemu ya kulea nafsi za wanafunzi katika kushirikiana baina yao”.

Akafafanua kuwa: “Ratiba hii inasaidia kujenga uwelewa na uwajibikaji kwa jamii, kwa kuandaa mambo mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi, yanayo jenga moyo wa kujitolea na kushirikiana na jamii”.

Taasisi ya Ain pia imeshiriki katika soko hilo, kwa ajili ya kujenga misingi ya kibinaadamu kwa wanafunzi na kuwafanya wawe na moyo wa kusaidia watu katika jamii, wanafunzi wanaoshiriki kwenye soko hilo wamesema kuwa jambo hilo linawajenga kiimani na kuwapa moyo wa kuendelea na masomo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: