Maonyesho ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Kufa

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu, inafanya maonyesho ya Qur’ani kwa njia ya picha katika chuo kikuu cha Kufa, kwenye eneo la bustani za kitivo cha uhandisi kukiwa na matawi mengi.

Maonyesho hayo ni sehemu ya harakati za mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi, ulioanza hivi karibuni, na utekelezaji unafanyika kwenye chuo kimoja baada ya kingine na kwenye Maahadi za mkoa wa Najafu, kwa lengo la kuongeza utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa wanafunzi wa chuo.

Maonyesho haya yamehusisha matawi mengi, miongoni mwa matawi hayo ni:

  • Tawi la kauli za wanachuoni kuhusu Qur’ani tukufu na tafsiri yake.
  • Tawi la harakati kuu za Majmaa ya Qur’ani na ufafanuzi wake.
  • Tawi la harakati kuu za Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi kilicho pita.
  • Tawi la maonyesho ya msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa nakala zote, ambao ni moja ya mafanikio kwani ndio msahafu wa kwanza kuchapishwa Iraq chini ya usimamizi wa raia wa Iraq.
  • Tawi la vitabu vilivyo andikwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu Ashrafu.
  • Tawi la miradi ya Qur’ani kwa wanafunzi wa Dini, nao ni miongoni mwa miradi yenye mafanikio, kwani wamenufaika mamia ya wanafunzi wa Dini.
  • Tawi la kazi za kuonekana (video), kama vile: (Vipindi vya Qur’ani, ripoti, visomo, mihadhara..), na vinginevyo.

Kumbuka kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi unahusisha harakati mbalimbali, miongoni mwa harakati hizo ni: Kufanya nadwa za Qur’ani ndani ya vitivo na vitengo vya vyuo, kufanya mashindano ya Qur’ani katika usomaji na kuhifadhi, maonyesho ya Qur’ani kwa picha, maonyesho ya uandishi wa Qur’ani, semina za usomaji wa Qur’ani kwa usahihi na kanuni za tajwidi na ratiba ya kuendeleza walimu wa vyuo vikuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: