Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil inafanya vipindi vya redio

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya tawi la Baabil kwa kushirikiana na redio Babelon imeandaa vipindi vya redio vya kila wiki chini ya anuani isemayo (Qur’ani na Itra).

Vipindi hivyo vinaandaliwa na Dokta Hassan Maamuri, na kurushwa mubashara kwenye redio ya Babelon kila siku ya Jumapili saa mbili jioni, vipindi hivyo vinahusu aya za Qur’ani zinazotaja familia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu cha kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inajukumu la kufundisha Qur’ani na kuchangia katika ujenzi wa jamii yenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika sekta tofauti za Qur’ani tukufu.

Kumbuka kuwa tawi la Maahadi litaendelea kufanya vipindi vya redio na luninga, na jambo hilo limeingizwa kwenye mkakati wake mpya wa mwaka (2022m) na kuanza kuutekeleza kupitia program ya (Qur’ani na Itra) inayo lenga kufundisha Qur’ani katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: