Shule ya sekondari ya wasichana Al-Ameed inaendesha zowezi la kutoa chanjo ya Korona

Maoni katika picha
Shule ya sekondari ya wasichana Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imepokea ugeni wa madaktari kutoka idara ya chanjo za virusi vya Korona, kwa ajili ya kuwachanja wanafunzi.

Dokta Ahmadi Kaabi rais wa kitengo tajwa amesema “Jopo la madaktari limetembelea shule ya sekondari ya wasichana Al-Ameed, kwa ajili ya kutoa maelekezo ya afya pamoja na kutoa chanjo ya virusi vya Korona kwa wanafunzi waliokua hawajachanja siku za nyumba na baada ya wao kukubali chanjo”.

Akabainisha kuwa: “Kama inavyo julikana, kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinawapa umuhimu maalum wa kupewa chanjo ya Korona walimu na wanafunzi, hususan baada ya wanafunzi kuruhusiwa kurudi shuleni”.

Akaendelea kusema: “Opresheni hii ni sehemu ya mkakati wa shule za Al-Ameed wa kuboresha mazingira ya elimu kila nyanja, hususan nyanja ya afya kulingana na mazingira ambayo taifa linapita kwa sasa na dunia kwa ujumla, ya maambukizi ya virusi vya Korona, shule za Al-Ameed zimeweka mpango maalum wa kutoa chanjo ya Korona kwa walimu na wanafunzi wake”.

Kumbuka kuwa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya kinafanya kila kiwezalo katika kulinda afya za walimu na wanafunzi kwa kuwapa chanjo pamoja na huduma za afya na matibabu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: