Mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu umegawa zaidi ya sahani elfu (30) za chakula kwa jina la bibi Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa kimetoa zaidi ya sahani elfu (30) za chakula kwa mazuwaru wa malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Ijumaa na mchana wa Alkhamisi (2 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (6 Januari 2022m) katika kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Rais wa kitengo Mhandisi Aadil Hamami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Mgahawa umezowea kuandaa na kugawa chakula kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku, usiku wa Ijumaa huwa tunagawa chakula kingi zaidi, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya mazuwaru, chini ya mkakati maalum wa utoaji wa huduma, kuna matukio ambayo husadifu siku hizo, likiwemo tukio la kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) mwaka huu limesadifu usiku wa Ijumaa”.

Akaendelea kusema: “Tulianza kujiandaa kwa ajili ya siku hii muda mrefu, nayo inakamilisha huduma tulizotoa kwenye maombolezo sawa na haya kwa mujibu wa riwaya mbili za mwanzo, lakini mara hii imesadifu katika siku rasmi ya mapumziko na usiku wa Ijumaa, katika kuhuisha kumbukumbu hiyo tumefanya kazi kubwa, ikiwa ni pamoja na kugawa milo mitatu ya chakula kwa mazuwaru (asubuhi, mchana na jioni), bila kusahau matunda, vitafunwa, chai na juisi, sambamba na kugawa maji wakati wote, kazi imefanywa mfululizo tangu asubuhi na mapema hadi usiku mwingi, tutaendelea hadi kesho siku ya Ijumaa”.

Akamaliza kwa kusema: “Chakula kinapikwa ndani ya jiko la mgawaha na kuwekwa kwenye vifungashio (takeaway), na kukigawa kupitia vituo maalum vya ugawaji wa chakula vya nje, huku wanaume na wanawake wakisimama kwenye mistari kwa ajili ya kupata chakula”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: