Kumbukumbu ya kifo cha mkarimu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Fatuma Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Siku ya Ijumaa mwezi tatu Jamadal-Aakhar (1443h) sawa na tarehe (7 Januari 2022m), ni siku ya kuomboleza kifo cha Mkarimu wa Mtume mtukufu (s.a.w.w) na mke wa kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalibu (a.s), mtukufu wa wanawake wa duniani Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu inayosema kuwa alifariki (a.s) mwezi tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa 11 hijiriyya, kwa mujibu wa riwaya hiyo anakua bibi Zaharaa (a.s) alibaki hai baada ya kifo cha baba yake kwa muda wa siku tisini na tano.

Bibi Fatuma (a.s) baada ya kifo cha baba yake aliishi siku za kuhesabika, zilizo jaa huzuni, majonzi na maudhi.

Imepokewa katika kitabu cha Kashful Ghumma na vingine kuwa: alipo karibia kufa (a.s), alimuambia Asmaa binti Umaisi amletee maji, akatawadha na inasemekana akaoga kisha akajipuliza marashi, halafu akavaa nguo mpya, kisha akamuambia Asmaa kuwa: Mtume (s.a.w.w) alipokaribia kufa, alikuja Jibrilu (a.s) akiwa na Kafuur kutoka peponi akaigawa mafungu matatu, moja la Mtume na linguine la Ali na lingine la kwangu na kulikua na dirham arubaini.

Akasema: Ewe Asmaa niletee manukato ya baba yangu uniwekee chini ya kichwa changu, nikamuwekea. Halafu akajifunika nguo yake akasema: niache kidogo kisha unite nisipo kujibu ujue nimeshakwenda kwa baba yangu.

Nikakaa kidogo kisha nikamwita, hakuitika. Nikaita ewe binti wa Muhammad Mustwafa, ewe binti wa mtukufu zaidi kushinda watu wote waliobebwa na wanawake, ewe binti wa mtu bora zaidi aliyetembea katika ardhi, ewe binti wa mtu aliyefika karibu na Mola wake kwa kiwango cha upinde au karibu zaidi ya hapo.

Hakujibu, anasema: Nikafunua nguo usoni kwake, nikakuta amesha aga dunia, nikamkumbatia na kumbusu huku nikisema: Fatuma utakapofika kwa baba yako Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) mfikishie salam kutoka kwa Asmaa binti Umaisi.

Imamu Ali (a.s) alisimamia mazishi yake, baada ya kumaliza alisimama na kusema: “Amani iwe juu yako ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kutoka kwangu na kwa binti yako aliyelala jirani yako, aliyefanya haraka kuungana na wewe, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Subira yangu imekua ndogo, muili wangu wasisimka, ispokua msiba mkubwa ulikua kutengana na wewe, nilikulaza kwenye mwanandani wa kaburi lako, nafsi yako ikatengana na mimi. Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, hakika nimerejesha amana na huzuni yangu itadumu, siku zangu zitakua za mateso hadi Allah atakapo nileta katika nyumba ambayo wewe upo, binti yako atakuambia yaliyofanywa na umma wako.

Kisha akasoma beti (a.s) zisemazo:

Kadri utakavyokua karibu na umpendae mtatengana + hakuna watakao ishi bila kutengana.

Hakika kumkosa kwangu Fatuma baada ya Ahmadi + ni dalili kuwa mpenzi hawezi kudumu.

Pamoja na kuwa na umri mfupi, Maisha yake yalijaa kheri na baraka, alikua kiigizo chema kwa wanaume na wanawake, alikua binti wa mfano, mke wa mfano na mama wa mfano, ndio maana akawa mbora wa wanawake wa ulimwenguni.

Hivi ndivyo ukurasa wa Maisha ya Fatuma Zaharaa (a.s) ulivyo fungwa na kuanza ukurasa wa maisha ya peponi, na kuendelea kuwa hai milele katika historia ya kiislamu na kuwa mfano mwema wa kuigwa milele na milele.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: