Mbele ya malalo ya mwanae na ndugu yake (a.s) mawakibu ya kuomboleza inahuisha kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Malalo mbili takatifu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) jioni ya leo siku ya Ijumaa mwezi tatu Jamadal Aakhar 1443h na usiku wake, imeshuhudiwa maukibu ya waombolezaji ya pamoja ambayo hufanywa kila mwaka katika kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, huku mazingira halisi yakisema: Mwenyezi Mungu akuze malipo yenu kwa kufiwa na mbora wa wanawake Mtoto wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), hili ni tukio kubwa lililo umiza nyumba ya Mtume mwaka wa kumi na moja hijiriyya.

Matembezi yamefanywa katika mtindo wa maukibu (kundi) ambalo imeshiriki idadi kubwa ya waombolezaji, baadhi yao walikua wamebeba jeneza la kuigiza la mtoto wa Mtume (s.a.w.w), matembezi yao yalianzia katika barabara inayoelekea kwenye malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuwa ndio kituo cha kwanza cha uombolezaji.

Halafu wakaelekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili, wakipita katikati ya makundi makubwa ya mazuwaru na waombolezaji wanaotembea kwa miguu, huku wanaimba kaswida za kuomboleza hadi wakafika katika malalo ya mfiwa Abu Abdillahi Hussein (a.s) na kumpa pole kwa kufiwa na mama yake Fatuma Zaharaa (a.s).

Maukibu hiyo ni muendelezo wa maukibu ya jana, imefanywa chini ya uratibu wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, ambacho kimeweka utaratibu maalum wa matembezi hayo, washiriki wa matembezi wametoka ndani na nje ya mji wa Karbala, jambo hili ni utamaduni uliozoweleka katika kuomboleza kwa mujibu wa riwaya zinazo taja tarehe ya kifo chake (a.s).

Kumbuka kuwa ushiriki hauishii katika maukibu hii peke yake, kulikua na mawakibu za wanawake pia, ambazo zimeratibiwa na kuongozwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu, sambamba na kuweka mazingira mazuri kwenye kila barabara inayo tumiwa katika matembezi ya maukibu, kuanzia mwanzo hadi mwisho wa matembezi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: