Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya majlisi za kuomboleza kifo cha Zaharaa (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Ijumaa mwezi (3 Jamadal Aakhar 1443h) imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Swidiqah Twahira Fatuma Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu.

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kufunguliwa kwa Qur’ani, kisha Shekhe Dhiyaau Al-Abadi kutoka kitengo cha Dini akatoa mawaidha, akazungumza kuhusu Maisha ya mbora wa wanawake wa duniani (a.s) na nafasi yake mbele ya baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w), na mume wake kiongozi wa waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), pamoja na nafasi yake katika uwanja wa elimu na usimamiaji wa Dini takatifu, huku akitoa Ushahidi wa hadithi za Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watakatifu (a.s), aidha ameongea kuhusu dhulma alizo fanyiwa na kisa cha kifo chake.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma utenzi wa kuomboleza ulio amsha hisia za huzuni kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kuwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), katika kila sehemu ya dunia wanaomboleza msiba huu mkubwa wa kifo cha mtoto wa Mtume Fatuma Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: