Kumtambua bibi Zaharaa (a.s) anuani ya maombolezo ya wanawake

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya, kwa kushirikiana na kituo cha Swidiqatu Twahirah (a.s) imeratibu majlisi ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s) na kuangazia historia yake tukufu.

Majlisi imefanywa ndani ya ukumbi wa kituo na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kundi la waombolezaji, baada ya kufunguliwa majlisi kwa Qur’ani tukufu, ulifuata mhadhara uliotolewa na mmoja wa wahadhiri wa idara, mada yake ilikua inasema: (kumtambua bibi Zaharaa a.s), ameongea kuhusu nafasi yake na daraja lake, akasema kuwa ni mtu asiyejulikana undani wake ispokua na Mwenyezi Mungu, Mtume na Maimamu (a.s), yeye amebeba siri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hakika kumjua huleta mafanikio duniani na akhera, hakika anatokana na Mtume Muhammad (s.a.w.w), na ametambulishwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Aidha imesomwa kaswida ya kuomboleza iliyotaja dhulma alizo fanyiwa, na mwisho ikasomwa dua na kumpa pole Imamu wa zama.

Kumbuka kuwa idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake imeweka utaratibu maalum wa kuhuisha na kukumbuka matukio yaliyowasibu Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na familia zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: