Kumaliza uwekaji wa dhahabu na mina kwenye dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Yanafanyika maandalizi katika kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi matukufu na milango katika Atabatu Abbasiyya, na kuunganisha sehemu zilizo wekwa madini katika dirisha la bibi Zainabu (a.s), baada ya kumaliza kutengeneza sehemu iliyotiwa dhahabu na mina kama ilivyo pangwa.

Sehemu zilizo kamilika kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Sayyid Naadhim Ghurabi aliyotoa kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kuwa: “Imehusisha ufito wa maandishi ya Qur’ani na mashairi pamoja na ufito wa mapambo unao tenganisha baina yake, tumeweka dhahabu kwa kutumia mitambo ya kisasa, ambayo imeonyesha mafanikio makubwa kwenye madirisha yaliyo tengenezwa na kitengo chetu”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kumaliza kazi ya utiaji wa dhahadu inafata kazi ya kuunganisha sehemu hizo kwa kuweka kila kipande mahala pake kwenye umbo la mbao, kwa ajili ya kukamilisha hatua ya mwisho”.

Akabainisha kuwa: “Utiaji wa dhahabu (ya kiwango cha 24 na usafi wa 99.9) umehusisha fito za mapambo na ufito wa maandishi ya ziara, na uwekaji wa mina umehusisha sehemu ya chini ya maandishi ya shairi na Qur’ani, na sehemu zingine pia zimetiwa dhahabu”.

Kumbuka kuwa kazi inaendelea sehemu zote, yanafanyika matengenezo katika kila sehemu ya madini au mbao, kazi inakaribia kukamilika kwani inafanywa mfululizo bila kusimama, kwa ajili ya kuhakikisha inakamilika kwa wakati chini ya utendaji wa watumishi wa malalo ya msimamizi wa mwenye malalo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: