Hospitali ya Alkafeel inaendeleza mafanikio ya upandikizaji wa mifupa

Maoni katika picha
Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limetangaza kufanikiwa kwa opresheni ya kupandikiza mfupa kwenye paja la mguu wa kushoto wa mgonjwa mwenye umri wa miaka zaidi ya ishirini, mgonjwa huyo alikua na tatizo la mfupa kutokana na ajali ya gari.

Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo Dokta Osama Abdulhassan amesema kuwa: “Tumefanikiwa kufanya upasuaji kwa kutumia teknolojia ya kufunga vyuma, baada ya kuchukua kipande cha mfupa kwenye mguu wa kushoto na kuupandikiza kwenye paja la kushoto la mgonjwa mwenye umri wa miaka (26)”.

Akabainisha kuwa: “Mgonjwa alikua amepoteza (sm10) ya mfupa wa paja kutokana na ajali ya gari”.

Akafafanua kuwa: “Upasuaji umefanywa awamu mbili, ya kwanza tulipandikiza mfupa wa kutengenezwa, na hatua ya pili tulichukua mfupa halisi kutoka mguu wa kushoto na kuuweka kwenye paja”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hudoa huduma daiama kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa, chini ya madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya taifa, jambo ambalo limeifanya iweze kutoa ushindani mkubwa kwa hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa mbalimali kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa walio katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: