Zaidi ya wanafunzi 80 wanashiriki kwenye mitihani ya mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu katika mji wa Karbala

Maoni katika picha
Zaidi ya wanafunzi (80) wameshiriki kwenye mitihani ya mradi wa kuhifadhi Qur’ani tukufu, iliyofanywa chini ya usimamizi wa idara ya Tahfiidh chini ya Maahadi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Mitihani hii inalenga kuangalia uwezo wa kuhifadhi kwa wanafunzi, chini ya mkakati maalum wa mradi wa kuhifadhisha Qur’ani, ikiwa ni pamoja na mitihani ya mzunguko kwa wanafunzi wa tahfiidhi ili kuwafanya wasome zaidi walicho hifadhi.

Tambua kuwa mitihani hiyo imefanywa katika mji wa Karbala, na wameshiriki wanafunzi wengi wa tahfiidhi kutoka hapa mkoani na mikoa mingine.

Kumbuka kuwa idara ya tahfiidhi hufanya semina mbalimbali za Qur’ani, makumi ya wanafunzi wamehitimu semina hizo kwa kuhifadhi idadi tofauti za mazujuu.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo muhimu cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya chenye jukumu la kufundisha Qur’ani, na kuchangia katika kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: