Kuratibu semina za Qur’ani kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kike

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutoa mihadhara ya Qur’ani kwa watumishi wa kike, kwa ajili ya kuongeza maarifa na elimu ya Qur’ani.

Bibi Fatuma Sayyid Abbasi Abdu-Hashim ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Masomo hayo yanatolewa kupitia semina za Qur’ani, kwa lengo la kuongeza maarifa kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani jambo hilo ni muhimu kwao”.

Akaongeza kuwa: “Semina inahusisha masomo ya Qur’ani kwa watumishi wa kike katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafundishwa usomaji sahihi na hukumu za usomaji, chini ya wakufunzi waliobobea katika masomo hayo, tunatarajia kufundisha idadi kubwa ya watumishi kama itakavyo wezekana, tumewagawa katika nyakati mbili, wakati wa asubuhi na jioni, ratiba yetu haiwazuwii kutekeleza wajibu wao kazini”.

Akaendelea kuwa: “Wanafundishwa usomaji wa Qur’ani na tafsiri ya baadhi za aya, pamoja na mafundisho ya kimalezi, pia wanapewa majaribio na mitihani kwa ajili ya kukazia maarifa ya vitu wanavyo fundishwa”.

Kumbuka kuwa idara ya Qur’ani tawi la wanawake chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya, hufanya harakati mbalimbali zinazo lenga kufundisha Qur’ani katika jamii, aidha inafanya miradi mingi ya kieneo, ikiwa ni pamoja na kuhifadhisha Qur’ani tukufu kwa njia ya kuhudhuria darasani na kwa mtandao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: