Kituo cha tafiti za ki-afrika (Dirasaat-Afriqiyya) kinafanya nadwa kuhusu mambo ya Afrika

Maoni katika picha
Kituo cha tafiti za ki-afrika (Dirasaat-Afriqiyya) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya nadwa kuhusu mambo ya Afrika, ndani ya ukumbi wa kituo cha Murtadha katika mkoa wa Najafu, na kuhudhuriwa na wanafunzi wa kiafrika na wasomi wa mambo ya Afrika.

Mkuu wa kituo Shekh Saadi Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya semina nyingi zinazofanywa na kituo chini ya anuani isemayo: (Harakati za kizalendo Afrika.. kwa mfano, harakati ya majimaji ya Kenya), nadwa hiyo imeongozwa na Dokta Sanaan Swadiq Hussein kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya, mto mada alikua Dokta Swadiq Hassan Sudani mkufunzi wa historia ya Afrika katika chuo kikuu cha Bagdad/ kitivo cha adabu, ameongea kuhusu uanzishwaji wa harakati ya majimaji, malengo yake, shughuli walizo fanya na mengineyo”.

Akaongeza kuwa: “Nadwa imeshuhudia majadiliano mazuri kutoka kwa watafiti na wanafunzi wa kiafrika”.

Nadwa imehitimishwa kwa kumpa zawadi mtoa mada na washiriki, wote kwa ujumla wameonyesha umuhimu wa nadwa hii, kutokana na mchango wake katika tafiti za mambo ya Afrika.

Kumbuka kuwa nadwa hii ni sehemu ya mfululizo wa nadwa mbalimbali zinazofanywa na kituo kuhusu mambo ya Afrika yenye mchango mkubwa katika uwanja wa elimu na tafiti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: