Jambo hilo limefikiwa kupitia kongamano la Qur’ani lililofanywa ndani ya ofisi za Maahadi katika mkoa wa Najafu, chini ya kauli mbiu isemayo: (Qur’ani tukufu ni msingi wa Aqida na ngome ya jamii) na anuani isemayo: (kuboresha mazingira ya usomaji wa Qur’ani tukufu), wahadhiri wa nadwa hiyo walikua ni walimu waliobobea katika sekta tofauti za Qur’ani tukufu.
Mkuu wa Maahadi Ustadh Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kongamano la Qur’ani ni sehemu ya mradi mkubwa wa Qur’ani unaoendeshwa na Maahadi, unaangalia namna ya kuboresha mambo yanayo husiana na Qur’ani, kwa kutumia njia za kisasa chini ya wabobezi wa mambo hayo, kama vile Dokta Basim Al-Abadi, Ustadh Abulfadhil Jafari, Sayyid Hassanaini Halo, Dokta Ahmadi Najafi, Sayyid Ridhwaa Nasrudini Mussawi, Sayyid Ahmadi Zamili na Ustadh Faisal Matwar”.
Akaongeza kuwa: “Kwenye kongamano hilo mitazamo na fikra tofauti zimewasilishwa, zinatakiwa kufanyiwa kazi kwa ajili ya kuboresha mazingira ya usomaji wa Qur’ani, maazimio yafuatayo yamefikiwa:
- Kuunda kamati itakayosimamia usomaji wa Qur’ani na walimu wa sauti na Naghma.
- Kuandaa selebasi moja ya sauti na naghma za Qur’ani.
- Kuandika kitabu cha mafunzo ya kiroho na kimalezi kwa wasomaji wa Qur’ani tukufu”.
Washiriki wameeleza umuhimu wa kongamano hilo, kutokana na mchango wake mkubwa katika kuboresha sekta ya Qur’ani na kuendeleza wasomaji wa Qur’ani tukufu.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu, imezowea kufanya makongamano na warsha za kitafiti, ili kuendeleza sekta ya Qur’ani na kuboresha mazingira ya usomaji na elimu kwa ujumla, sambamba na kutatua changamoto za wasomaji wa Qur’ani na mahafidhu.