Kundi la watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi limetembelea malalo ya baba yake (a.s) na ofisi za Maraajii-Dini katika mji wa Najafu

Maoni katika picha
Idara ya Tablighi chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetembelea malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) ikiwa na kundi la watumishi wa malalo ya mwanae Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuhuisha utii kwake na kumpa pole kwa kifo cha Swidiqah Twahirah bibi Fatuma Zaharaa (a.s), sanjari na kutembelea ofisi za Maraajii-Dini watukufu katika mji wa Najafu.

Kiongozi wa Idara hiyo, bwana Muhammad Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii ni sehemu ya ratiba iliyo andaliwa kwa kushirikiana na idara ya mahusiano ya ndani katika kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, yenye lengo la kujenga hali ya mawasiliano kati ya watumishi wa malalo tukufu na malalo zingine, sambamba na kujenga ukaribu baina ya watumishi, hivyo ziara hii ni sehemu ya kuonyesha thamani ya ushirikiano wao kwetu”.

Akaongeza kuwa: “Safari yetu haikuishia kwenye kutembelea malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) peke yake, bali tumetembelea ofisi za Maraajii-Dini watukufu, kwa ajili ya kutambuana na kuimarisha ushirikiano pamoja na kusikiliza nasaha na maelekezo yao, bila kusahau utukufu wao na mapenzi yetu kwao na umuhimu wa kushikamana na nasaha zao”.

Akafafanua: “Tulikua na kikao kirefu na Marjaa Dini mkubwa Ayatullah Shekh Bashiru Najafiy, baada ya kukaribishwa amezungumza maneno mazuri na nasaha Madhubuti, ametaja neema na baraka kubwa wanazopata watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), akasisitiza umuhimu wa kupambika na tabia nzuri wakati wa kuhudumia mazuwaru watukufu, akafafanua utukufu wa kutoa huduma katika eneo lile takatifu, na utukufu wa wahudumu, akasema kuwa wanatakiwa kushukuru kwa kupata nafasi hiyo, ili idumu neema ya kutoa huduma”.

Mwisho wa kikao hicho mheshimiwa ameshukuru ugeni huo kutembelea ofisi yake na kukutana nae, akasifu uhodari wao wa kutembelea wanachuoni na akawataka waendelee kufanya hivyo, halafu akawaombea dua.

Ugeni huo pia umemshukuru sana kwa mapokezi mazuri, na mawaidha muhimu aliyotoa, wakamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awalinde Maraajii-Dini watukufu, ambao ni nguzo madhubuti za taifa la Iraq na raia wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: