Muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya amekua mgeni rasmi katika chuo kikuu cha Alkafeel na ametoa muhadhara mzuri

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimemualika muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kadhimiyya Mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yaasini kwenye ratiba ya mradi wa Qur’ani katika vyuo vikuu na Maahadi unaoendeshwa na Maahadi ya Qur’ani katika mji wa Najafu, chini ya uratibu wa ofisi ya saikolojia na malezi vyuoni.

Shekh Aali Yaasini amefurahisha idadi kubwa ya watumishi wa chuo, akiwemo rais wa chuo Dokta Nurisi Dahani na wakuu wa vitivo, walimu na wanafunzi, kwa muhadhara elekezi wenye mafunzo ya Qur’ani, aliotoa kwenye nadwa yenye anuani isemayo: (Aya za Qur’ani katika utukufu wa mashahidi na mujahidina).

Shekh ameongea kuhusu malezi na jamii katika kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, na kueleza utukufu wake, aidha ametaja umuhimu wa kusoma Qur’ani na kudumu nayo, watu wajiepushe sana kukihama kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, aidha tunatakiwa kufanyia kazi mafundisho yake sambamba na mafundisho ya hadithi za Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kufuatia kauli yake isemayo: (Mimi nakuachieni vizito viwili kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumbani kwangu), hali kadhalika ameongea kuhusu jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na aina zake pamoja na malipo ya mujahidina.

Mwisho wa nadwa kulikua na maswali na maoni mbalimbali ambayo yalionyesha ushiriki hai wa wajumbe.

Pembeni ya nadwa hiyo wanafunzi wa chuo kutoka kitivo cha udaktari na uuguzi, walifanya maonyesho ya picha na kugawa vipeperushi, vilivyo kua vimeandikwa aya za Qur’ani na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), kama sehemu ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha bibi Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: