Maahadi ya Qur’ani tawi la Hindiyya chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya semina maalum ya Qur’ani kwa waimbaji wa mimbari za Husseiniyya.
Semina imefanywa karibu na malalo ya watoto wa Hassan (a.s), chini ya wakufunzi waliobobea katika usomaji wa Qur’ani, nayo ni miongoni mwa harakati za Qur’ani zinazo fanywa na tawi ndani ya wilaya, zenye lengo la kufundisha vizito viwili vitakatifu.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Hindiyya, hufanya semina za Qur’ani kwa lengo la kujenga utamaduni wa kusoma Qur’ani hapa wilayani.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni moja ya kituo cha Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, kwa lengo la kutoa elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kuandaa jamii yenye uwelewa wa Qur’ani kwenye sekta zote.