Kitengo cha maadhimisho na mawakibu kimeanza kufanya maandalizi ya kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimeanza kufanya maandalizi ya kuratibu shughuli za mawakibu za kuomboleza na kutoa huduma zitakazo shiriki katika kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina (a.s) aliyekufa mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar.

Hatua ya kwanza ya maandalizi hayo ni kupokea maombi ya ushiriki kutoka kwa viongozi wa mawakibu za ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na kuwaingiza kwenye orodha maalum kisha kuwapangia utaratibu wa namna ya ushiriki wao.

Baada ya kumaliza hatua hiyo utaandaliwa mpango kazi maalum, kwa kila shughuli ya uombolezaji, idadi kamilia ya mawakibu za uombolezaji itajulikana na kupangiwa ratiba ya kuingia na kutoka, sambamba na kubainisha barabara watakazo tumia katika matembezi yao, kila maukibu itapewa ratiba yake, na kuhakikisha zinafanya shughuli zao bila kuingiliana baina yao au kutatiza shughuli za mazuwaru.

Aidha Maukibu za kutoa huduma pia zitawekewa utaratibu wao, sambamba na kupangiwa maeneo ya kutolea huduma kwa kuzingatia kanuni za afya.

Tambua kuwa kazi hizi hufanywa kwa kushirikiana na askari wa mkoa wa Karbala, vitengo vya ulinzi na usalama na vitengo vya kutoa huduma katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: