Kumaliza kutengeneza dari la mbao za mapambo kwenye dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango mitakatifu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimekamilisha utengenezaji wa dari la ndani kwa mbao za mapambo, kwenye dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), imebaki kazi ya kupaka rangi na matengenezo ya mwisho.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo Sayyid Naadhim Ghurabi, akaongeza kuwa: “Kazi ya kutengeneza dirisha la bibi Zainabu (a.s) inaendelea vizuri, na leo mafundi selemala wamemaliza kutengeneza kazi za mbao ambazo ni miongoni mwa vitu vilivyo ongezwa kwenye dirisha jipya, na havikuwepo kwenye dirisha la zamani, hakika kazi hiyo imebadilisha muonekano wa dirisha kabisa, sio kwenye uzuri wa muonekano tu bali hata uimara pia”.

Akaongeza kuwa: “Dari linamambo makuu yafuatayo:

  • - Ufito wa maandishi ya Qur’ani ukifuatiwa na vyumba vya madirisha kwa ndani, imeandikwa surat Nuur kamili kwa hati ya Thuluthu-Murakabu, urefu wa ufito ni (m3,87) na upana (m2,89) na kimo chake (sm64), maandishi yanaurefu wa (sm36) katika eneo lote la ufito lenye ukubwa wa (m13.89), sehemu iliyobaki kuna ufito wa mapambo ya rangi uliozunguka upande wa juu na chini.
  • - Ufito wa mapambo ya maandishi ukifuatiwa na maandishi ya surat Nuur, umezunguka pande zote za dirisha, kwa umbo la upinde wenye urefu wa (sm66), imewekwa nakshi na mapambo ya kiislamu, katikati yake kuna maandishi yasemayo (Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamtakia rehema Mtume, enyi mlioamini mtakieni rehema na amani), imeandikwa sehemu ya urefu na kurudiwa upande wa pili, kwenye eneo lenye ukubwa wa (m3,16) na urefu wa (sm60), upande mfupi sehemu ya mlango wa dirisha imepanbwa na kunakshiwa ili kuweka muonekano mzuri, ukitoa ufito ulioandikwa aya isemayo (Sema sikuombeni malipo juu yake ispokua kuwapenda watu wa karibu), hali kadhalika maandishi hayo yamerudiwa upande wa pili kwenye eneo lenye ukubwa wa (m1,42) na urefu wa (sm60).
  • - Mapambo na nakshi za mbao yanatenganisha dari la paa na sehemu tuliyotaja awali, yenye urefu wa (sm23), na imezunguka dirisha pande zote, kwa urefu wa (m3,16) na upana wa (m2,16), aina hii ya mapambo imewekwa kwa mara ya kwanza kaika umbo hili.
  • - Paa lenye umbo la mstatiri lenye urefu wa (m3,05) na upana wa (m2,06), nalo limetengenezwa na ubao uliopambwa vizuri, umewekwa katikati ya kubba na umegawanyika sehemu kumi na mbili na jumla ya (mbavu 12), ujazo wake ni (sm100) na urefu (sm35) katikati yake kuna pambo la kuwakawaka, pambo limezungukwa na vipande vilivyo andikwa (ewe Zainabu) vya umbo la pembe nne kwa hati ya Kufi, vipande vingine vimewekwa mapambo mazuri ya kupendeza, vipande vyote vimefungwa kwa ufundi na weledi mkubwa”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi hii imefanywa kwa ubora mkubwa sawa na kazi ya utengenezaji wa vipande vya nje ya dirisha”.

Akamaliza kwa kusema “Vipande hivyo vimetengenezwa kwa mbao za Saaji-Burma, na sehemu ya chini zimetumika mbao za Baluti nyeupe, simsim, Baluti na Zaan, kwa kutumia mikono na baadhi ya muda kwa kutumia vifaa, limekua na muonekano mzuri kutokana na rangi ya mbao na mapambo pamoja na rangi za mbao na mapambo, sambamba na nakshi zilizo wekwa kwenye vipande vingine na maandishi, matumizi ya mbao yamezingatia vipimo maalum kila sehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: