Kituo cha turathi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa kitabu chenye maudhui zilizokua hazijawahi kuandikwa kwenye kitabu chochote

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Najafu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa kitabu kipya kwa anuani isemayo: (Kubaini wakati na kibla katika Raudhat-Bahiyya), miongoni mwa uandishi wa Shekhe Muhammad bun Ali bun Naswiru-Dini Annajafiy ajulikanae kama (Mwalimu wa Rashti), aliyekufa kwaka 1334h, na kuhakikiwa na Shekhe Swalahu Alkhuzai.

Mkuu wa kituo Ustadh Ahmadi Ali Alhilliy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitabu hiki ni moja ya misingi muhimu ya kifiqhi katika kueleza maswala ya wakati na kibla kutoka kwenye kitabu cha Sherehe ya Llum’a-Dimishqiyya, yatafuata machapisho mengine kuhusu turathi za mji wa Najafu na wanachuoni wake na athari zao”.

Akafafanua kuwa: “Kitabu hiki kinamaudhui zake maalum, ambazo ni ngumu kuzikuta kwenye vitabu vingine, muandishi wa kitabu hiki alikua anafundisha kitabu cha (Raudhat-Albahiyya katika sherehe ya Lum’atu-Demishqiyya) cha Shahidi wa pili aliyekufa mwaka wa (965h), na vitabu vingine vya fiqhi katika mji wa Najafu hadi akapewa jina la mwalimu (Almudarrisu)”.

Akasisitiza kuwa: “Ni muhimu kwa watu wa Najafu kuchapa upya kitabu hiki kutokana na kuharibika kwa sababu ya kukaa muda mrefu, tena kwa uhakiki mpya na muonekano mpya, kwa kufanya hivyo ndio kutumikia elimu na kuitukuza, ndio tukaamua kufanya kazi hiyo”.

Kumbuka kuwa kitabu hiki kilikua na kurasa (300) zilizo na maudhui zisizopatikana kwenye vitabu vingine, kimefafanua vizuri maoni ya muandishi, sambamba na kueleza kwa undani aya na hukumu za wakati na kibla, na kubainisha baadhi ya misemo inayo husiana na maudhui..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: