jirani na Raudhwat Nabii (s.a.w.w) zaidi ya mazuwaru elfu 60 wamefanyiwa ziara kwa niaba ndani ya siku za Fatwimiyya

Maoni katika picha
Idara ya Teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya imetandaza kuwa dirisha la ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel -mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya-, imesajili zaidi ya watu (elfu 60) walio omba kufanyiwa ziara katika ziku za Fatwimiyya, siku za kukumbuka kifo cha bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya ya tatu, wamefanyiwa ziara kwa niaba Jirani na Raudhwat ya baba yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mji wa Madina.

Kiongozi wa idara tajwa Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Ameer amesema “Ziara kwaniaba ni miongoni mwa huduma zinazo tolewa na mtandao wa kimataifa Alkafeel, huduma hiyo inashuhudia ongezeko kubwa la watu wanaojisajili siku baada ya siku, hususan katika kipindi hiki, miongoni mwa ziara kwa niaba ambazo hufanywa ni ziara ya bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya zote tatu, mwezi nane Rabiul-Thani, mwezi kumi na tatu Jamadal-Uula na mwisho riwaya ya tatu katika mwezi huu wa Jamadal-Aakhar”.

Akaongeza kuwa “Kuna ratiba maalum katika kila kipindi cha maombolezo, ambayo hutangazwa siku tatu au nne kabla ya kuanza kila ziara, na hufanywa ziara kwa niaba na watu wanaojitolea katika mji wa Madina pamoja na kuswali rakaa mbili na kusoma dua kwa ajili ya watu walio jisajili kupitia mitandao yetu ya lugha tofauti ambazo ni (Kiarabu – Kiswahili – Kijerumani – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Kiurdu – Kifaransa)”.

Akahitimisha kuwa: “Kulikua na muda mrefu wa kutandaza ziara hizo, ili kutoa nafasi ya kupokea maombi mengi zaidi, asilimia kubwa ya watu waliojisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malezia, Australia, Moroko, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Aljeria, Afghanistan, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Finland, China, Ailend, Honkon, Japani, Falme za kiarabu, Sudani)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: