Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza mradi wa kuhifadhisha juzuu la mwisho la Qur’ani, zaidi ya wanafunzi sabini (70) wa shule za msingi wanashiriki.
Shekhe Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya amesema: “Maahadi inaendesha miradi mbalimbali, ukiwemo mradi wa kuhifadhi juzuu la thelathini la Qur’ani tukufu, na tunajitahidi kuandaa wanafunzi ili waweze kuhifadhi Qur’ani yote ndani ya muda mfupi kama ilivyo pangwa na Maahadi, hivi karibuni tutaanza harakati nyingine Inshallah.
Akaongeza kuwa: “Mradi unalenga kufundisha usomaji, kuhifadhi na kutafakari Qur’ani tukufu, sambamba na kupambana na mashambulizi ya kifikra, na kufanyia kazi kauli ya kiongozi wa waumini (a.s) isemayo: (Atakaesoma Qur’ani akiwa muumini kijana Qur’ani itachanganyika na nyama na damu yake)”.
Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu ni kituo muhimu katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inajukumu la kufundisha Qur’ani tukufu na kuandaa jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Qur’ani na kufanya tafiti za kielimu katika sekta zote za Qur’ani tukufu na fani zake.