Kufanya mitihani ya mwisho katika mashindano ya Fatwimiyya kwa wanawake

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumamosi (11 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (15 Januari 2022m), imefanya mitihani ya mwisho kwenye mashindano ya Fatwimiyya kwa mwaka wa kwanza, ambapo mada zake zilijikita kwenye (khutuba ya Fadakiyya) ya bibi Zaharaa -a.s-.

Kiongozi wa idara bibi Taghridi Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mashindano hayo yalitangwazwa sambamba na kumbukumbu ya kuomboleza kifo cha bibi Zaharaa (a.s), tulitoa muda wa maandalizi na leo tunafanya mitihani ya mwisho ambayo imejitokeza idadi kubwa ya washiriki kutoka ndani na nje ya mji wa Karbala, mashindano haya yamefanyiwa kwenye shule za Alkafeel zilizopo kwenye mikoa tofauti”.

Akaongeza kuwa: “Majibu ya washiriki wote yatawasilishwa kwenye kamati maalum ya majaji, kwa kuzingatia masharti ya shindano yaliyo tangazwa, ili kuchagua majibu sahihi na kupata washindi, kama ikitokea wamegongana tutapiga kura ili kupata washindi watatu, majina ya washindi yatatangazwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s).

Tambua kuwa mashindano yanahusu mambo matatu: (Maelezo kuhusu ardhi ya Fadak, Madhumuni ya khutuba ya Fadakiyya iliyotolewa na bibi Zaharaa (a.s), hadithi takatifu za Mtume (s.a.w.w) zinazo eleza utukufu wa Swidiqah Twahirah (a.s).

Kumbuka kuwa lengo la mashindano haya ni kubaini dhulma aliyofanyiwa bibi Zaharaa (a.s) na namna alivyo simama kudai haki yake, pamoja na kuonyesha msaada mkubwa unaotolewa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kila kitu kinacho husiana na bibi Zaharaa (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: