Kutokana na kifo cha bibi mtukufu msiba umetangazwa

Maoni katika picha
Mazingira ya majonzi na huzuni yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Ummul-Banina mama yake Abulfadhil Abbasi na ndugu zake (a.s), aliyekufa siku kama ya kesho Jumatatu (13 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (17 Januari 2022m).

Atabatu Abbasiyya na korido zake zimewekwa mapambo meusi, kuta zake zimefungwa mabango meusi yaliyo andikwa maneno ya kuombeleza kutokana na msiba huo, na kutaja nafasi ya mama huyo mtakatifu (a.s).

Shughuli hiyo ni sehemu ya ratiba ya uombolezaji iliyoandaliwa kwa ajili ya msiba huu uliotokea mwaka (64) hijiriyya, wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanaomboleza msiba huo kila sehemu ya dunia.

Kama kawaida katika kuomboleza tarehe zilizotokea vifo vya Ahlulbait (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya kuomboleza msiba huu.

Kumbuka kuwa mwezi kumi na tatu Jamadal-Aakhar mwaka wa (64h) alifariki mama mtukufu Ummul-Banina mke wa kiongozi wa waumini (a.s), aitwae Fatuma bint Hizam Alkilabiyya Al-Aamiriyya, na akapewa jina la Ummul-Banina kwa sababu alikua na watoto wanne wakiume na wote waliuawa katika vita ya Twafu huko Karbala, wakimnusuru bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), alifia katika mji wa Madina na akazikwa kwenye makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: