Alasiri ya leo siku ya Jumatatu (13 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (17 Januari 2022m) zimefanyika shughuli za awamu ya saba ya shindano la kaswida bora ya Umudiyya kuhusu Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya usimamizi wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: (Ummul-Banina na mwezi wa familia mwenye kujitolea na bwana wa utukufu), sambamba na kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s).
Shindano limefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuhudhuriwa na makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu na kundi la wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo, pamoja na watumishi na washairi walioshinda kwenye mashindano, bila kusahau viongozi wa Dini na sekula kutoka ndani na nje ya Karbala.
Shindano lilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya bwana Muslim Aqiil Shabaki, ukafuata ujumbe kutoka kamati ya maandalizi, uliowasilishwa na rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyasiri, miongoni mwa aliyosema ni:
“Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatilia umuhimu kufanyika kwa shindano la shairi bora la umudiyya, shindano hilo limefanywa mara sita mfululizo, lakini kutokana na majanga yaliyolikumba taifa ya mashambulizi ya magaidi wa Daesh katika baadhi ya miji, pamoja na janga lililotokea duniani miaka miwili ya hivi karibuni la Korona, shindano hilo lilisimama, lakini -Tunamshukuru Allah- tumefanikiwa kufanya awamu ya saba kupitia kitengo cha habari na utamaduni kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Alkafeel”.
Akaongeza kuwa: “Shindano hili zaidi ya kaswida (70) zimeshiriki kutoka nchi tofaui za kiarabu, ambapo kaswida kumi zimeshinda”, akabainisha kuwa: “Tumeandika chapisho la nakala za zamani za kaswida zilizo shinda, tutaongeza na kaswida zilizo shinda katika awamu hii”.
Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi uliowasilishwa na rais wa kamati hiyo Dokta Sarhani Jafaati, kisha akatangaza majina ya washindi, halafu usomaji wa mashairi ukaanza ndani ya haram ya mbeba bendera (a.s), washindi wakaitwa kwenye jukwaa kusoma kaswida zao mmoja mmoja, waliitwa kwa mpangilio ufuatao:
Mshindi wa kwanza: Hauraa Ali Hamimi kutoka Saudia, kaswida yake inasema (Kivuli katika sifa ya ta-awili).
Mshindi wa pili: Shaakir Rikani Ghazi kutoka Iraq, kaswida yake inasema (Amesimama kwenye jurfi-muniyaat).
Mshindi wa tatu: Masaar Riyaadh kutoka Iraq, kaswida yake inasema (Hivi ndio nilivyo ona).
Mshindi wa nne: Hussein Ali Aali-Ammaar kutoka Saudia, kaswida yake inasema (Baridi huficha kiu).
Mshindi wa tano: Ali Makiy Ali Sheikh kutoka Saudia, kaswida yake inasema (Mto hufichuliwa na kiu).
Mshindi wa sita: Naasir Mula Hassan Zain kutoka Baharain, kaswida yake inasema (Baina ya hatua na tone lililokatazwa).
Mshindi wa saba: Sefu Hassan Hussein Dhabihawi kutoka Iraq, kaswida yake inasema (Ahadi ya kupaa).
Mshindi wa nane: Hassan Amiinu Ra’di kutoka Lebanon, kaswida yake inasema (Posta ya farati ina aina).
Mshindi wa tisa: Aadil Alwani Hussein Swawiri kutoka Iraq, kaswida yake inasema: (Uwezo wa Abbasi).
Mshindi wa kumi: Hamza Hussein Abbadi kutoka Iraq, kaswida yake inasema: (Kuangaziwa mwanga).
Mwisho washairi walioshinda, kamati ya majaji na waliochangia kufanikiwa shindano hili la awamu ya saba, wakapewa zawadi.