Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Alasiri ya leo siku ya Jumatatu (13 Jamadal-Aakhar 1443h) sawa na tarehe (17 Januari 2022m) wamefanya maukibu ya kuomboleza na kumpa pole mtumishi wa kaka yake Imamu Hussein (a.s) na kiongozi wa jeshi Abulfadhil Abbasi (a.s), haku mazingira halisi yao yakisema: Mwenyezi Mungu akuze malipo yako ewe bwana wetu ewe Abulfadhil Abbasi kutokana na msiba huu.

Shughuli za uombolezaji ni utamaduni uliozoweleka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ni kawaida kuhuisha tarehe walizofariki Maimamu watakatifu (a.s) kwa kufanya matembezi ya kuomboleza kuanzia Atabatu Abbasiyya tukufu hadi kwenye haram ya Imamu Hussein (a.s), lakini katika kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) ratiba hubadilika, watumishi wa malalo ya Imamu Hussein (a.s) hufanya maukibu kubwa na kupokewa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) ndani ya haram yake takatifu.

Kisha hufanywa majlisi ya kuomboleza ya pamoja na kuimba kaswida na tenzi zinazo taja utukufu wa bibi huyo kihistoria, bibi aliyetumia Maisha yake yote katika kumlea Hassan na Hussein (a.s) mabwana wa vijana wa peponi, na akajitolea watoto wake kwenda kumtumikia Imamu Hussein na kumlinda, historia haijua mwanamke aliyekua muaminifu kwa watoto wa mume wake na kujitolea watoto wake kwa ajili ya kumlinda mtoto wa mume wake ispokua mama huyu mtukufu.

Ataba mbili tukufu tangu asubuhi ya leo zimeshuhudia mawakibu za waombolezaji na makundi ya waumini wakimiminika kuja kuomboleza msiba huo.

Aidha Atabatu Abbasiyya tukufu imevaa vazi leusi na kufanywa majlisi za kuomboleza ndani ya haram tukufu ambapo inazungumzwa historia ya mama huyo mtakatifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: